John 12:12-16

12 aSiku iliyofuata umati mkubwa uliokuwa umekuja kwenye Sikukuu walisikia kwamba Isa angekuja Yerusalemu. 13 bBasi wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema, “Hosana!”
Kiebrania kusema Okoa, basi likawa neno la shangwe.

“Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!”

“Amebarikiwa Mfalme wa Israeli!”

14 dIsa akamkuta mwana-punda akampanda, kama ilivyoandikwa,
15 e“Usiogope, Ewe binti Sayuni;
tazama, Mfalme wako anakuja,
amepanda mwana-punda!”

16 fWanafunzi wake Isa mwanzoni hawakuelewa mambo haya, lakini Isa alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka kuwa mambo haya yalikuwa yameandikwa kwa ajili yake na alitendewa yeye.

Copyright information for SwhKC